Articles by "Top 10"
Showing posts with label Top 10. Show all posts
Android ni mfumo endeshi unaotumika zaidi katika simu na tablets kwa sasa duniani kote kutokana na urahisi wake na wingi wa applications zinazoweza kutumika katika mfumo huo kutoka Play Store.

Mfumo endeshi huo kutoka Google kwa sasa umeliteka soko la mifumo endeshi ya simu na kuwaacha mbali sana wapinzani wake kama iOSWindowsBlackberry na Symbian.
Wengi tunaotumia vifaa vinavyotumia mfumo endeshi huu wa Google lakini kuna baadhi ya vitu hatuvifahamu kabisa. Leo Riyadi bhai nakuletea orodha ya mambo kumi ya kustaajabisha yanayohusiana na mfumo endeshi huu.

Mambo 10 usiyoyafahamu kuhusiana na Android

1. Android haikugunduliwa na Google

Mfumo endeshi wa android uligunduliwa na Andy RubinChris WhiteNick Sears na Rich Miner kipindi hicho ikiwa inafahamika kama Android Inc mwaka 2013. Baadae Android ilinunuliwa na Google ambayo iliendelea kuumiliki mfumo endeshi huo mpaka sasa. Google walinunua mfumo endeshi huo kutoka kwa Android Inc August 2005 kwa dau la $50 milioni.

2. Google waliachia Android rasmi mwaka 2007

Mfumo endeshi wa Android uliachiwa rasmi na kampuni ya Google mwaka 2007 na kuanza kutumika katika smartphones na kamera. Hapo awali mfumo endeshi huo ulitengenezwa maalumu kwa ajili ya kamera.

3. Android ilitengenezwa maalumu kwa ajili ya Kamera

Android kwa mara ya kwanza ilitengenezwa kwa ajili ya smartcameras, ila google waliona ubora wa mfumo endeshi huo katika simu na kuamua kuamishia katika simu na kuleta mapinduzi makubwa sana katika soko.

4. HTC Dream ni simu ya kwanza kuanza kutumia mfumo endeshi wa Android

Simu ya kwanza kuanza kutumia mfumo endeshi wa Android ilikuwa ni HTC Dream ambayo iliachiwa rasmi mwaka 2008 na kampuni ya HTC. Simu hiyo ilianza kwa kutumia toleo la android 1.0 na iliboreshwa mpaka kufikia toleo la android 1.6. Hapo mwanzo android ilipigwa madongo sana kuwa mfumo endeshi uliokosa mwingiliano mzuri na mtumiaji, japo baadae maoni hayo yalibadilika na kuiona android kama inaleta mapinduzi katika soko.

5. Android inatumika na zaidi ya watu bilioni moja duniani kote

Makamu wa Rais wa Google katika kitengo cha Android bwana Sundar Pichai, alitangaza kuwa kwa sasa mfumo endeshi wa android unatumika na zaidi ya vifaa bilioni 1 duniani kote katika nchi zaidi ya 190.

6. Majina ya matoleo ya Android yamekuwa yakipewa majina ya vyakula vyepesi au majina ya majangwa

Ukiacha android 1.0 na 1.1, matoleo mengine yote ya mfumo endeshi huu yamekuwa yakifuata majina ya vyakula vyepesi (sweet treats) au majangwa. Mfano wa majina hayo ni kama CupCake, Donut, Eclair, Froyo, Gingerbread, Honeycomb, Ice Cream Sandwich, Jelly Bean, Kitkat, Lollipop, Marshmallow na android N ambayo bado haijatoka rasmi.

7. Majina ya matoleo ya Android yanafuatana kwa Alphabets

Ukiangalia kwa makini majina ya matoleo ya mfumo endeshi huu utagundua yanafutana kwa alphabets.

8. Android ni Open Source (Huru na wazi)

Google wanatoa mfumo endeshi huu bure kwa watengenezaji na watumiaji wa mfumo endeshi huu na kuyapa nafasi makampuni mengi kutumia mfumo endeshi huo bila malipo. Hii inachangia sana kukua kwa mfumo endeshi huu.

9. Soko la wazi la kuuza na kusambaza Applications

Google ni mwanachama wa  Open Handset Alliance (OHA), Android inawapa watumiaji wake ruhusa ya kutumia source code zake bure bila malipo. Hii imepelekea kuzuka kwa matoleo tofauti mengi ya Android ambayo hayahusiani moja kwa moja na Google.

10. Google inafaidika kwa kiasi kikubwa na Android

Kupitia matangazo katika baadhi ya app zinazouzwa katika Play Store, google inatengeneza kiasi kikubwa cha pesa kwa mwaka kuliko kampuni yoyote kwa sasa.
Soko la bidhaa za umeme (Electronic Gadgets) linabadilika kila kukicha huku makampuni tofauti yakijaribu kuonyeshana ubabe katika fani hii. Kuanzia na bidhaa kama simu, Kamera, TV, magari pamoja na kompyuta zote zimekuwa zikiboreshwa kila siku.


Wengi wamekuwa wakiuliza na kuomba ushauri juu ya mashine gani nzuri sokoni kwa sasa ili wanunue. Leo nimeamua kuwaletea orodha kamila ya Laptop 10 kali zinazobamba kwa sasa katika ulimwengu wa kiteknolojia. Orodha hii imepangwa kulingana na ubora wa mashine husika kwa kuangalia vitu kama Processor, Memory, Diski Hifadhi, Umbo na shape yake bila kusahau bei na maoni ya watumiaji.

1. Dell XPS 13 Ultra Book

Mashine hii kwa sasa ndio inaongoza katika soko kwa kuwa mashine kali zaidi kwa matumizi yote.
CPU: Intel Core i5 – i7 | Graphics: Intel HD Graphics 520 – Intel Iris Graphics 540 | RAM: 4GB – 8GB | Screen: 13.3-inch FH (1,920 x 1,080) – QHD+ (3,200 x 1,800) | Storage: 128GB – 256GB SSD
Faida
  • -Display nzuri ya kisasa
  • -Uzito mdogo, wembamba wa kutosha
  • Skylake processor
  • Bei nzuri
Hasara
  • Web Cam haipo kati
  • Batri linakufa kirahisi zaidi

2. Asus ZenBook UX305

Mashine kali zaidi ya MacBook kwa bei nafuu kutoka Asus. Ikiwa na viwango vyote vya kuitwa UltraBook. Faida kubwa ya mashine hii ni kukaa na chaji kwa muda mrefu zaidi.
CPU: Intel Core Intel Core M3-6Y30 – M7-6Y75 | Graphics: Intel HD Graphics 515 | RAM: 8GB | Screen: 13.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) – QHD+ (3200 x 1800) IPS display | Storage: 256GB – 512GB SSD

3. Razer Blade Stealth

Kwa wale jamaa zangu wapenda magemu hapa ndio mahala pao. Ikiwa imetengenezwa maalumu kwa ajili ya wapenzi wa magemu, mashine hii inakuja na keyboard inayoweza kubadilisha rangi ya kila key. Kuanzia vitufe vya A mpaka Z kila kimoja kinaweza kuwaka taa na rangi yake bila kusahau processor ya Kaby Lake Core i7 kutoka Intel.
CPU: Intel Core i7 | Graphics: Intel HD Graphics 620 | RAM: 8GB – 16GB | Screen: 12.5-inch, QHD+ (2,560 x 1,440) – 4K (3,840 x 2,160) IGZO LED-backlit multi-touch | Storage: 128GB – 1TB SSD

4. Samsung Notebook 9

Uzuri mkubwa wa mashine hii upo kwenye bei na huduma inazotoa. Bei yake ni nafuu sana ukilinganisha na uwezo wa mashine husika.
CPU: 2.3GHz Intel Core i5-6200U | Graphics: Intel HD Graphics 520 | RAM: 8GB | Screen: 13.3-inch, FHD (1,920 x 1,080) LED anti-reflective display | Storage: 256GB

5.  Surface Book

Ukiachana na ukali wa bei, mashine hii ilibidi ishike nafasi ya kwanza kwenye orodha hii kwa kuwa ndio mashine kali zaidi kutoka mwaka 2016 inayotumia Windows 10. Katika mshine hii Microsoft waliacha kazi wakafanya kazi katika kutengeneza umbo na kioo cha mashine hii. Pia uwezo wake wa kutumika kama tablet unaifanya mashine hii kuwa mpinzani wa kweli wa MacBook kama lengo la watengenezaji lilivyokuwa.
CPU: Intel Core i5 – i7 | Graphics: Intel HD graphics 520 – Nvidia GeForce graphics | RAM: 8GB – 16GB | Screen: 13.5-inch, 3,000 x 2,000 PixelSense Display | Storage: 128GB – 256GB PCIe3.0 SSD

6.  HP Spectre

Hapa najua nimewafurahisha mashabiki wa HP, mashine hii ni ya pili kwa ubora kwa mwaka 2016 ukiacha HP Chromebook 13 ambayo ni ya bei nafuu zaidi kwa sababu ni Chrome Book (Mashine inayotumia mfumo endeshi wa Chromium kutoka Google). HP Spectre ni moto wa kuotea mbali linapokuja suala la kuhimili mikikimikiki ya kila siku.
CPU: Intel Core i5 – i7 | Graphics: Intel HD Graphics 520 | RAM: 8GB LPDDR3 SDRAM | Screen: 13.3-inch FHD (1,920 x 1,080) IPS UWVA WLED | Storage: 256GB – 512GB SSD

7.  MacBook (2016)


Apple wametengeneza mashine hii wakiwa na lengo la kuwafurahisha mashabiki wake wanaopenda mashine zenye umbo zuri zaidi na zinazokaa na batri muda mrefu. Ikiwa na Processor ya Intel Skylake Core M mashine hii inakuja na teknolojia ya kisasa ya USB-C. Hauna sababu ya kuikosoa mashine hii kama wewe ni mtu unayekwenda na wakati.
CPU: Intel Core m3 – m5 | Graphics: Intel HD Graphics 515 | RAM: 8GB | Screen: 12-inch, 2304 x 1,440 LED-backlit IPS display | Storage: 256GB – 512GB SSD

8. Lenovo Yoga 900


Mashine hii kutoka kwa wakali Lenovo inakuja katika matoleo mawili, kama wewe ni mpenzi wa mashine nyembamba zaidi nakushauri ununue toleo la Lenovo Yoga 900S.
CPU: 2.5GHz Intel Core i7-6560U | Graphics: Intel Iris Graphics 540 | RAM: 8GB – 16GB | Screen: 13.3-inch QHD+ 3,200 x 1,800 IPS display | Storage: 512GB – 1TB SSD

9. MacBook Pro (15-inch, Late 2016)

Ukiachana na kipengere cha bei, mashine hii ilitakiwa ishike nafasi ya kwanza au ya pili ikichuana na Microsoft Surface Book. Kwa miaka mingi sasa MacBook Pro imekuwa chaguo la madesigner na madeveloper wengi. Hii ni kutokana na uwezo wake mkubwa katika kufanikisha kazi nzito bila matatizo yoyote. Ikiwa na Retina Display mashine hii inavotia kila dakika kuiangalia.
CPU: Intel Core i7 | Graphics: AMD Radeon Pro 450 – 460 | RAM: 16GB | Screen: 15.4-inch Retina (2,880 x 1,800) LED-backlit IPS | Storage: 256GB – 2TB PCIe SSD

10. Lenovo ThinkPad X1 Yoga

Kwa miaka ya hivi karibuni Lenovo imekuwa ikitengeneza mashine za kuaminika katika soko. Ikiwa na processor ya Intel Core i5 na Core i 7 mashine imefunga orodha hii kwa ubora.
CPU: Intel Core i5 – i7 | Graphics: Intel HD Graphics 520 | RAM: 8GB | Screen: 14-inch, FHD (1,920 x 1,080) – WQHD (2560 x 1440) IPS touchscreen | Storage: 180GB – 512GB NVMe SSD
Je wewe unatumia Ipi , au ipi imekuvutia zaidi niachie maoni yako hapo chini