Articles by "Instagram"
Showing posts with label Instagram. Show all posts
Baada ya Instagram kufanya majaribio ya uwezo mpya wa kupost picha au video zaidi ya moja kwenye post moja, sasa uwezo huo umekuja live kwenye programu zote za instagram. Mtumiaji ataweza kupost picha au video 10 kwa mara moja kwenye post moja ya mtandao huo wa Instagram. Ili kupost picha nyingi kwa wakati mmoja uta bofya kitufe kipya kilichop upande wa kulia juu ya picha wakati unataka kupost kisha hapo utapata uwezo wa kuanza kupost picha 10 kwenye post moja. Kumbuka kuwa kwa sasa instagram imeweka uwezo wa kuweka maneno (caption) kwenye picha moja tu hivyo usitegemee kila picha itakuwa na maneno yake bali picha zote zitatumia (caption) moja.

Sehemu hiyo mpya tayari imeshanza kutoka kwa watu wote wenye programu za Instagram za iOS na Android hivyo pale unapona toleo jipya la programu hiyo ni vyema ukaupdate ili kuweza kupata sehemu hiyo mpya
Instagram ni moja ya mtandao wa kijamii ambao unatumiwa na watu zaidi ya billioni moja. Kwenye playstore peke yake instagram imekuwa downloaded zaidi ya mara billioni moja.

Watu wengi wanatumia instagram kila siku lakini yapo mambo mengi mapya ambayo wengi wetu bado hatuja yafahamu. Leo ntaelezea mambo matano mapya ambayo instagram wameanzisha ndani ya mwaka 2017 na baadhi ni ya mwaka 2016.

Live Stories Sasa kwenye Instagram utaweza kujichukua au kuji record live na watu ambao wame kufollow wakawa wanakuona live. Watu wataweza ku comment huku video yako ikiwa live. 

Saved Post

Instagram inatumbua kwamba watu wapo busy, sasa inakupa uwezo wa ku save post ambayo ungependa uje uingalie baadae. Ku save post ni kitu rahisi sana. Unacho takiwa kufanya ni kubonyeza alama ya bookmark ambayo inakuwa chini ya post. Tazama picha chini kuelewa zaidi

Instagram Strories

Stories ni kitu ambacho watu wengi sana wanasema Instagram ame copy kutoka snapchat. Stories inakusanya matukio yako yote ya siku moja na watu wanaweza wakaona vitu vyote ulivyofanya siku nzima kwa pamoja. 

Event Channels

Sasa unaweza kucheck matukio kama concert za wasanii mbalimbali kupitia instagram. Hii channel inakusanya video kali kutoka kwenye matamasha mbalimbali. Kwa sasa Event Channel inaonekana kwa watu wa marekani tu. Instagram wanajitahidi kuisambaza event channels ziweze kuonekana ulemwenguni kote. 

Account Mbili

Kujua kuhusu account tatu za instagram unaweza tembelea link chini HAPA
Habari na karibu tena katika ukumbi huu jana nilizungumzia [jinsi ya kutumia account 3 za instagram katika simu moja] lakini leo nimekuja na njia mpya ambayo itakuwezesha kutumia zaidi ya akaunti tano za instagram bila kuweka application nyingine kama OGinsta+ ili usitoke patupu katika makala hii kuwa makini na kufuata maelekezo hapa chini


Jinsi ya kufanya ili utumie zaidi ya akaunti moja kwenye app ya instagram


Hakuna haja ya kuwa na application mbili au tatu za Instagram kwenye simu mmoja fungua Instagram yako then fanya kama unataka kulog out kuna sehemu utaona imeandikwa "ADD ACCOUNT" utaweza kulog in na account nyingi unavyotaka.
 unachokakiwa kufanya ni ku-swich account tu. Soma na hii pia [ Jinsi ya kupata followers wengi instagram]

Kama unaswali niachie kwenye sanduku la maoni hapo chini nami nitajitahidi kukujibu usisahau kushare makala hii.