TRENDING NOW

As salaam aleikumndugu zangu kutokana na kila mmoja anakuwa na sheria zake kwaajili yake na watu wake binafsi nimeanzisha blog hii kwaajili ya kuwasaidia watu wa aina zote zaidi blogger's hasa wanaotumia lugha ya kiswahili lakini kwa masikitiko makubwa nimeona sheria zangu zikivunjwa wazi kabisa jambo ambalo likanatisha tamaa kuendelea kufanya mambo makubwa zaidi, nimeweka sheria kwa wale wanao kopi makala zangu hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/about.html nimeweka masharti rahisi sana katika sheria hiyo lakini watu wamekuwa wagumu kuelewa.

mpaka umeamua kukopi makala kutoka sehemu moja kupeleka kwako bila shaka umefahamu ni ugumu kiasi gani kuandaa makala mpaka ikiwa na msaada kwa watu wengine hivyo ili tusivunjane moyo katika kusaidiana naomba tujitahidi kufuata sheria za blog hii kwani sifanyi ili kupata pesa lakini nafanya hapa ili kuwasaidia watu wengine kama unahitaji kukopi makala kutoka katika blog hii soma hapa kabla ya kukopi https://riyadibhai.blogspot.com/p/about.html soma sheria za huduma zangu hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/terms-of-service.html soma sheria mama za mtandao huu hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/privacy-policy.html kama unamalalamiko soma hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/blog-page_29.html kama utakubaliana na sheria hizo basi wasiliana nami hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/contact.html
As salaam aleikum ndugu yangu Ni ngumu kidogo kuamini kama inawezekana Jambo hili kutokana na sifa ya ulinzi mkali ulipo katika mtandao huu pendwa wa telegram ninapokwambia kujiunga bila namba ya simu sina maana kuwa ni rahisi sana ila niamini kuwa inawezekana tena inawezekana bila hata kutumia email yako
Kikubwa ni kuzingatia haya nitakayokueleza ili kufanikiwa katika zoezi letu hili la kujiunga na mtandao wa telegram bila kutumia namba yako ya simu
Hapa chini nimekuwekea video jinsi yakukamilisha zoezi letu itazame hapa chini

As salaam aleikum ndugu yangu Jifunze kila kitu, jifunze kila siku tuendelee na mpya yetu hii Hey Cortana, hii ni komandi ya sauti inayotumika kumwamsha Cortana ili aweze kukusaidia.

Matoleo ya zamani ya windows kama windows XP, windows Vista, windows 7 pamoja na windows 8 kulikuwa na msaidizi mzuri pale ulipokuwa unataka kutafuta baadhi ya vitu katika kompyuta yako au hata mtandaoni. Kikubwa ilikuwa ni kufungua sehemu ya kutafuta na kuandika unachotaka kutafuta, alafu unakaa pembeni kusubiria matokeo.

Teknolojia hiyo imetumika katika matoleo yote ya nyuma ya windows kabla ya windows 10, hali imekuwa tofauti kidogo katika windows 10. Windows 10 imekuja na msaidizi wa sauti anayejulikana kama Cortana. Je, Cortana ni nini hasa?

Cortana ni programu inayokuja na windows 10 inayokusaidia wewe mtumiaji wa kompyuta kutafuta kila kitu unachotaka katika kompyuta yako au mtandao kwa kuipa amri ya sauti tu. Mfano unataka kutafuta programu ya paint katika kompyuta yako, unachotakiwa kufanya ni kufungua programu yako ya cortana, pembeni tu ya Start menu kuna kama duara, huyo ndio Cortana, andika unachotaka kutafuta hapo au bonyeza alama ya kinasa sauti na toa amri yako kwa Cortana.

Kuna vitu vya kuzingatia kabla ya kutumia Cortana. Cha kwanza unatakiwa ufahamu kuwa programu hii kwa sasa inafanya kazi vizuri na lugha ya kiingereza, pili kama kitu hakipo katika kompyuta yako Cortana atajaribu kufungua kivinjari chako na kutafuta matokeo mtandaoni. Tatu, ni vizuri kuruhusu Hey, Cortana feature ili Cortana afanye kazi yake vizuri.

Jinsi ya kuseti Hey, Cortana feature ni rahisi, fungua sehemu ya search hapo pembeni ya start menu, alafu settings, alafu tafuta sehemu iliyoandikwa Note. Utaseti mipangilio kulingana na matakwa yako, baada ya hapo ni wewe na Cortana tu.
as salaam aleikum ndugu zangu wasomaji wa blog hii nimeshindwa kuwa hewani kwa kitambo kidogo kutokana na pirikapirika za kusaka mkate wa siku sasa nimerudi tena kidogo kuwajulia hali natumaini ni wazima kabisa tujifunze kila siku tujifunze kila kitu.

Ni rahisi sana kufahamu passwords za network zote za Wi-Fi ambazo kompyuta yako ya Windows ilishawahi kuungwa kwa kutumia Command Prompt (cmd) inayopatikana katika mfumo endeshi wa Windows.


Mara nyingi watu wanaohusika na IT au kitengo cha IT ndio wanaohusika zaidi na utoaji wa password za wifi katika maeneo yetu ya kazi, mashuleni au vyuoni. Mara nyingi huwa wanazificha passwords hizi hata kwa watumiaji wa kompyuta wa ndani.

Kama wewe ni mmoja wanaokumbwa na kadhia hii kutoka kwa IT wa ofisini au chuoni kwenu usitie shaka, hapa ndio mahala pake. Leo nitakuelekeza jinsi ya kupata password za wifi networks zote ulizowahi kujiunga kwa urahisi zaidi.

Kila mara tunapojiunga na WLAN katika kompyuta zetu, kuna profile maalumu kwa ajili ya WLAN hiyo huwa linatengenezwa katika kompyuta zetu bila ya sisi kufahamu. Profile hilo linakuwa na taarifa zote za muhimu zinazohusiana na network hiyo.

Njia hii inatumika hata kama upo Offline na haujajiunga kabisa katika network hiyo kwa wakati huo.

Jinsi ya kufahamu password za WiFi Network
Fungua Command Prompt kama Administrator, bonyeza Windows + X kufanya hivyo


Hatua inayofuata ni sisi kutambua profile zote za wlan zilizowahi kuhifadhiwa katika kompyuta zetu. Andika komandi ifuatayo katika cmd kisha bonyeza enter: netsh wlan show profile


Komandi hiyo itakuonyesha profile zote zilizowahi kuhifadhiwa katika kompyuta yako.

Baada ya kuona profile zote za WLAN ulizowahi kuunganishwa nazo, sasa ni wakati wa kuangalia password kwa kila pofile kwa kuandika komandi: netsh wlan show profile WiFi-name key=clear


Badilisha sehemu ya WiFi-name na weka jina la wifi unayotaka kuona password yake

Katika sehemu ya security settings, katika kipengere cha ‘key content’ utaona password za wifi husika.
As salaam aleiku, Watumiaji wengi wa barua pepe (e-mail) wanapoingia kwenye uwanja wa kutuma ujumbe katika akaunti zao ama iwe Gmail, Yahoo, Microsoft Outlook, Live Mail, na Mozilla Thunderbird, kuna sehemu inayoonesha CC na BCC.

Lakini wapo baadhi ambao wamekuwa hawaelewi nini maana ya hizo herufi na nini matumizi yake kuwepo hapo.

Maana ya CC na BCC

CCing inasimama badala ya ‘Carbon Copying‘ na BCCing inasimama badala ya ‘Blind Carbon Copying‘. Zote mbili, CC na BCC zinakuwezesha kuwatumia watu wengi kwa wakati mmoja ujumbe au mafaili unayokusudia kuwapelekea.

Kuona na kutumia CC au BCC ni pale unapofungua uwanja wa kutuma barua pepe yako sehemu ya kuandika barua pepe kwa unayemtumia ndipo utapoona hizo CC na BCC.
Yaani unaweza kuwatumia ujumbe kwa njia ya barua pepe watu 20 au zaidi kwa wakati mmoja bila ya kupata taabu ya kumtumia mtu mmoja mmoja; ni kitendo cha kuweka barua pepe zao kwenye kipengele cha BCC/CC na kuwatumia mara moja.

Pamoja na kufanana kwa kazi ya kuwatumia watu wengi kwa wakati mmoja, lakini kuna tofauti ndogo baina ya CC na BCC:-

Unapotumia njia ya ‘CC’ kuwatumia watu wengi ujumbe, ni kwamba kila mmoja ataweza kuona orodha kamili ya wapokeaji wengine waliotumiwa ujumbe huo; kila aliyetumiwa ataona na barua pepe za wengine waliotumiwa ujumbe kama wake.

Kama utahitaji kuwatumia watu wengi ujumbe wa aina moja na kila mmoja asijue mwingine aliyetumiwa basi matumizi ya ‘BCC’ yatakuhusu. Kupitia kipengele cha BCC kwenye barua pepe utaweza kuwatumia watu wengi lakini kila mmoja ataona ujumbe wake bila ya kujua kama kuna mwingine ametumiwa kama huo.

Credit : JamiiForums.com
As salaam aleikum, Kuna matumizi mengi sana ya kamera ya simu janja zetu ukiachana na yale tuliyo yazoea ya kupiga picha tu

Unajua kama kamera ya simu janja yako inaweza ikawa na matumizi lukuki ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kurahisisha maisha yako

1. Scan Nyaraka

Kamera ya simu janja yako pia inaweza ikawa ina’scan’ nyaraka tofauti tofauti. Pata picha unakuwa na ‘scanner’ ambayo ipo mfukoni kwako. Unaweza uka ‘scan’ vitu kama vile mikataba,risiti au kitu chochote kilichopo katika karatasi na unataka ukifanye kiwe kidigitali

Baada ya hapo unaweza ukaamua kutuma vitu hivyo katika barua pepe au unaweza ukavihifadhi katika mfumo wa PDF au JPG
Unataka ku’scan’ vitu?

Kwa iOS shusha(download) Evernote

Kwa Android shusha Google Drive ndani yake kuna kipengele cha ku’Scan’

2. Tumia Kamera Ya Simu Janja Yako Kama Mkalimani Wako

Teknolojia inabadilisha dunia kwa kiasi kikubwa sana miaka kadhaa iliyopita ningebisha kata kata kama jambo hili lingeweza kutokea. Hivi unajua unaweza ukatumia kamera ya simu yako ili kutafsiri lugha Fulani?

Kumbuka kuna maandishi huwa yanaandikwa na mara nyingi tunakuwa hatuyaelewi kwa mfano ukiwa katika mgahawa ikaja menyu yenye maandishi ya kigeni hapo ndipo huduma hii utakapo ona ubora wake

Ukiwa na App ya Google Translate, ambayo inaweza kutafsiri lugha 29 utafanikisha hilo kwa kuweka kamera mbele ya maandishi yaliyoandikwa na hapo App itafanya zoezi zima la kutafsiri kwenda katika lugha unayotaka

3. Tumia Kama Kamera Ya Ulinzi

Hivi ulishawahi kuwa na hamu ya kutumia kamera ya simu yako kama njia ya ulinzi? Labda una kamzigo kako pale ndani na unataka ukachunge. Ondoa shaka kuna App maalum ambazo zinakuwezesha kufanya hayo yote. App hizi hutumia kamera ya simu janja ili kugundua mwondoko wa aina yeyote (motion) na kisha kukutaariffu kupitia barua pepe (e-mail) yako

Kwa Android shusha App ya Silent Eye

4. Fuatilia Barcodes Za UPC

Wakati mwingine wakati ukiwa unafanya manunuzi ya vitu na ukawa huna uhakika kama unanunua vitu imara achana na ku Google, tumia kamera ya simu janja yako kuweza kuichunguza bidhaa hiyo.

Zile App ambazo zinamsaidia mtu ku’scan code’ za UPC zinampatia mtu taarifa za bidhaa katika kiganja chake kabisa. Ukiachana na taarifa kuhusiana na bidhaa bado utaweza kufananisha bei tofauti tofauti ya bidhaa hizo ili kujua kama umepewa bei nzuri au la

Kwa Android shusha App ya ShopSavvy Barcode and QR Scanner

5. Shangaa Anga

Hivi ushawahi kukaa usiku na ukawa unashangaa anga na ukaanza kujiuliza maswali kama baadhi ya vitu unavyoviona ni nyota au ni sayari zingine?
Sasa App ya Skyview kwa Android na iOs itakupa majibu yote

App hii inatumia kamera ya simu yako katika kukuonyesha jinsi anga ilivyo cha kufanya hapa wewe elekeza kamera ya simu janja yako katika anga.

Pia kama remote ya Tv au kisimbusi inasumbua unaweza kutumia kamera ya simu kuona kama remote hiyo inatoa mionzi au la kabla ya kuchukua hatua nyingine kama kubadili betri au kuitengeneza.Washa kamera ya simu,nyoshea kile kitaa cha remote kwenye kamera huku ukiwa una bonyeza vitufe kwenye remote.Utaona mwanga unawaka kwenye screen ya simu endapo kama remote ni nzima
As salaam aleikum ndugu zangu kwa wale blogger wa kongwe na wale wachanga ni kipindi kirefu tumesikia kuhusu neno adsense lakini kumekuwa hakuna Tija ya kulisikia tu neno Adsense, sababu hata baada ya kulisikia na kulijua kumekuwa ni vigumu kunufaika nalo kutokana na masharti yao.
Leo katika uchambuzi huu tuelewe kwanini Tunafikiri adsense wanaweza kukiweka kiswahili kati ya lugha zinazosapoti katika matangazo yao? 

Katika masiku ya hizi karibuni kampuni ya google imeboresha mtandao wake na huduma zake zote kwa ujumla kama kubadilisha muonekano wa dashbodi ya blogger.com, adword, adsense, youtube, google map, na hata adsense pamoja na mfumo wa upakiaji app wa google console, Lakini ukiangalia kipaumbele walichokipa kiswahili katika program zao ni kubwa mno kwa wale watumiaji wa google translate watakuwa wameona hili.

Kwa sasa lugha ya  Kiswahili imepata pendeleo la kutafsiriwa bila hata kuwa na muunganisho  wa data,hii ni fursa nzuri hasa pale utakapokuwa huna kifurushi.

Na kwa upande wa adsense ilikuwa kipindi cha nyuma ukifungua blog kisha kabla hujaifikia dashbodi ya blog ukachagua lugha ya kiswahili ndio iwe lugha mama ya blog yako google walikuwa wanakiondosha kipengele cha mapato katika blog yako.
 Lakini kwasasa kipengele hicho kinawekwa na google wenyewe hata kama utafungua blog yako kwa lugha ya kiswahili mwanzo mwisho, hii ni wazi siku za usoni blogger wanaotumia lugha ya kiswahili katika kuendesha blog zao wataanza kunufaika na adsense.

Hayo ndio machache kati ya mengi tuliyokuandalia siku ya leo endelea kuwa nasi ili kufahamu zaidi kuhusu ADSENSE

As salaam aleikum ndugu zangu wasomaji wa blog hii, kutokana na ombi la ndugu yetu Mfangavo kuhusu kujua jinsi ya kuweka sticky Ads basi nimeonelea niandae makala kamili ili tunufaike sote kwa pamoja wenda na wewe ulikuwa mmoja miongoni mwa watu waliohangaika kujaribu kufahamu jambo hili ila jitihada zako zikagonga ukuta, basi leo wacha nikupe suluhisho la jambo lako hilo kuwa makini katika usomaji wako ili upate kunielewa vema.

Hapa chini nimekuwekea code ambazo utaziweka katika blog yako katika upande wa Layout
<div style="left:0;position: fixed;text-align:center;bottom: 0px;width:100%;z-index:9999;"><center><a href="weka link ya tangazo lako">
<img src="weka code ya adsense hapa/ weka link ya picha ya tangazo lako">
</a></center></div>Twende sawa sasa hizo code unazoziona hapo juu ndio code tutacazo zitumia katika kukamilisha jambo letu hili copy code hizo  kisha nenda katika Layout ya blog yako kisha bonyeza Add a Gadget kama uovyoona katika picha hapo chini
 Kisha chagua Gadget iliyoandikwa HTML/JavaScript kama unavyoona pichani hapo chini, hapo ndio tutakapozikweka code zetu
 Kisha utaona uwanja ambao hauna kitu pacte/pachika code zako ulizozikopi hapo juu kwenye sehemu ya Title usiandike kitu, edit/rekebisha code zako kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa save
 Shabbash mpaka kufikia hapo utakuwa umefanikiwa kuweka Tangazo mnato/mgando katika blog yako hata kama mtu atafungua post ataliona tangazo hilo kama unavyoona pichani hapa chini


Bila shaka nimejitahidi kurahisisha katika kuelezea Jambo letu hili kama utakuwa kuna sehemu hujaelewa basi unaweza kuniachia maoni yako hapo chini nami nitajitahidi kukusaidia kadri nitakavyoelewa

makala hii Imeandikwa na Riyadi Bhai Sambaza kama Ilivyo kama unahitaji kukopi makala zetu zilizopo katika blog hii wasiliana nami kwa email RiyadiBhai@gmail.com


As salaam aleikum ndugu yangu Unapoanzisha tovuti, unataka kupata trafiki kubwa kadri iwezekanavyo. Unataka watumiaji (target audience) wako waweze kutembelea tovuti yako ili waweze kuwa wateja wako au watembeleaji wa kudumu baada ya kuona chapisho lako kwa mara ya kwanza na maudhui kwenye tovuti. Kwa hiyo, ni mambo gani ambayo mtu anaweza kufanya ili aweze kupata Trafiki ya uhakika ?

Naam, kuna mambo mengi ambayo unaweza kufanya ili kuhakikisha unapata watu uliowalenga (target traffic) kwenye tovuti yako. Hapa chini kuna mbinu 5 za kusaidia tovuti yako kufikia walengwa (target audience):

1. Weka lengo, na uwajue walengwa wako
Mtu hauwezi kuanzisha tu tovuti/blog bila ya kuwa na wazo kuhusu kitu utakacho wapatia watembeleaji wa tovuti. Lazima uwe na lengo la tovuti yako. Unataka kufikia nini na tovuti? Walengwa ni kina nani, watu ambao unataka kuwasiliana nao kupitia tovuti yako? Unapoweza kujibu maswali haya, ni wakati wa kuanzisha tovuti ambayo inalenga watazamaji wako.

Ukiweza kufafanua malengo yako, unaweza kuanzisha tovuti yenye maudhui yaliyo sahihi na maneno muhimu (keywords) ambayo yatatumika kama njia ya kuleta trafiki husika kwenye tovuti na google watakupa kipao mbele ukiwa hautachanganya mambo tovuti yako ni vema ikawa na maudhui maalum mfano ikiwa inazungumzia Tech basi usianze kuweka na muziki na udaku na mifano yake shika moja ili upate watembeleaji wa uhakika.


2. Maudhui yanayoendana na wasomaji

Njia rahisi ya kupata trafiki kwenye tovuti yako ni kupitia maudhui unayoweka kwenye tovuti. Je! Maudhui yako yanafaa? Kwa mfano, kama tovuti yako yote inahusu  muziki, basi kama una picha au taarifa muhimu ambazo zinahusiana na muziki ndio inakubidi uchapishe vitu vya namna hiyo, Ikiwa sio, huwezi kupata aina sahihi ya trafiki kwenye tovuti yako na kama hivyo, huwezi kufikia malengo yako.
Ikiwa unataka mafanikio zaidi, unapaswa pia kuwa na faili za video na sauti kwenye tovuti ili wasomaji wako waweze kuburudika na kupata taarifa zaidi. Hii itawawezesha wasomaji kuja kwenye tovuti yako mara kwa mara na kwa wingi.

3. Hakikisha tovuti yako inavutia


Ni muhimu kufanya tovuti yako iwe inavutia kupitia maudhui safi na maudhui yaliyopangwa vizuri. Je, tovuti imewekwaje upande wa maudhui? Tovuti ina kurasa ngapi? Ni aina gani za viungo vya nje (outside links)  vipo kwenye tovuti? Je! unaweka vitu kwenye tovuti mara kwa mara? Je, tovuti yako ina maingiliano? Vitu vyote hapo tulivyovieleza ni njia nzuri unazoweza kutumia kufanya tovuti yako iwe inavutia wasomaji wako. Wasomaji wako daima hupenda maudhui mapya mara kwa mara. Kumbuka kwamba injini za utafutaji pia zinapenda aina hii ya maudhui na hii ni njia nzuri ya kupata targeted audience kwenye tovuti.

4. Hakikisha tovuti inafunguka haraka


Hiki ni kipengele muhimu sana kwenye tovuti ambacho watu wengi hawakizingatii. Tovuti inapofunguka haraka, ni rahisi kupata trafiki zaidi. Kumbuka kwamba watu wachache sana ulimwenguni pote wana uwezo wa kufikia mtandao wenye kasi kubwa. Kwa hivyo, kasi ya kufunguka kwa tovuti, ni muhumu kwa wasomaji wako. Google pia inaziweka juu tovuti zinazofunguka kwa haraka zaidi kuliko zile ambazo hufunguka polepole.

5. Tumia Google Translate kwenye tovuti


Huenda usiwe na uwezo wa kuunda tovuti kwa kila lugha au nchi unayoilenga. Unaweza kutumia Google Translate kwenye tovuti yako ili wasomaji uliowalenga waweze kupata urahisi wa kupata ujumbe na habari kutoka kwenye tovuti yako. Hii ni nzuri zaidi kwa ajili ya startups na makampuni madogo ambayo yanataka kulenga wasomaji kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Bila shaka umepata mwanga kuhusu kuendeleza blog yako tuachie maoni yako usisahau kushare makala hii katika mitandao ya kijamii

As salaam aleikum Mswahili mwenzangu matumaini yangu uko poa kama mimi Alhamdulillah, leo tuangalie jinsi ya kubadilisha Version ya simu yako ya android wenda ukajiuliza kwanini nibadilishe Version ya android yangu naam inabidi tubadilishe kwasababu kuna app za muhimu wakati mwingine tunazihitaji lakini kutokana na version za simu zetu kuwa ni toleo la zamani tujikuta tunakosa uhondo huo. twende kwenye mada moja kwa moja tusipoteze muda sana, kama utakuwa na swali utaniuliza katika sanduku la maoni


Hatua ya kwanza download app inaitwa Root browers kutoka playstor nenda moja kwa moja na link hiyo hapa Download.

Baada ya kuifungua utaona files zimetokea nyingi hapo teremka chini na tafuta /angalia file lililoandikwa *System*

Fungua humo na teremka chini utaona kiji file kimeandikwa Build.prop
Angalia hicho maana vipo viwili kengine kanaitwa Build.prop.bak

Bonyeza Build.prop kisha itafunguka na options tano hapo angalia palipo andikwa RB text Editor

Ukisha bonyeza hapo itafunguka na utaona detail zote za simu sasa hapo utafanya chaguo lako kama unataka kubadili builder number, manufactures,  na mengineyo kwa version utashuka chini 
 kisha utaangalia palipo andikwa ro.build.version.release=[hapa itakuwepo version original ya simu kisha utaifuta na kuweka mpya]


NOTE; Hakikisha unaweka version isiyo zidi 7 usidhidishe zaidi ya hapo ili kuweka simu yako katika Latest isiwe imepitiliza italeta shida

kisha ukimaliza kufanya mabadiliko hayo utasevu kwa kubonyeza icon ya sevu iliyopo juu kabisa mkono wa kulia kialama chake kipo kama mfano wa hichi ki emoj 🏥

 kisha restart simu yako na nenda kaanglie version mpya uliyoweka katika settings kisha about phone
 na utaweza kudownload app bila kikomo kwa kutokuwa na kizuizi cha version

Kuna apps ambazo zinarun kwenye version latest tu, kwahiyo ukiweka version latest apps latest zitakubali. 

Kwa mfano Recharge king haiwezi kurun kwenye W3 tecno ila inarun kwenye k7 na k9 lakini ukibadilisha version kwenye w3 na kuweka 7 itarun bila shida.

Imeandikwa na Riyadi Bhai Sambaza makala kama ilivyo kama unahitaji kukopi makala hii soma hapa Copyright Policy Zingatia sheria za Blog hii Ahsante kwa Kutembelea Swahili Tech