Articles by "Tutorial"
Showing posts with label Tutorial. Show all posts
As salaam aleykum, Android ni mfumo (operating system) ambao ni maarafu sana kwa kuwa umefanikiwa kutumiwa kwenye vyombo vya kielectroniki kama simu, saa, tv, laptops, tablet na hata kwenye magari ya kisasa pia utakuta android.
Hii ina maanisha kama wewe una ndoto za kuwa android developer basi hujakosea kufanya maamuzi maana android ni mfumo ambao unatumiwa ulimwenguni kote na una endelea kukua kwa kasi kubwa na kutapakaa kwenye vitu vingi vya kielectroniki.
Ili kuweza kutengeneza Android app basi unapaswa kujua Java pamoja na XML(Extensible Markup Language). Wengi wetu tukishasikia tu Java basi tunakata tamaa. Lakini hutakiwi kuogopa maana Google wanajaribu kila siku kurahisisha utengenezaji wa android app.
Pia Google wana website inayo toa mafunzo jinsi ya kutengeneza android app pamoja na mifano mingi ambayo itakusaidia wewe kuweza kutengeneza app yako. Unaweza tembelea hiyo website kwa kutumia link chini
https://developer.android.com/index.html
Leo tutaangalia mambo yanayoitajika ili kuweza kutengeneza android apps.

Computer

Ili uweze kutengeneza android app unaitaji computer ambayo ina uwezo au sifa zifuatazo.

Kama una computer ya windows basi hakikisha computer yako ina sifa kama za hapo juu. Pia kama una Mac na linux basi hakikisha ina kidhi vigezo vyote kama hivyo hapo juu.

Android Studio


Android Studio ndio program inayotumia kama IDE (integrated development environment). Inamaanisha kwamba shughuli nzima ya kutengeneza android app, kuijaribu na hata kuiweka kwenye playstore itafanyikia kwenye android studio. Pia shughuli zote za ku test app yako zinafanyika ndani ya android studio.
Kwa kutumia android studio utaweza kutengeneza apps za simu, saa, android auto pamoja na android Tv. Android Studio imetengenezwa na Google ili kurahisisha shughuli za ku design android app. Unaweza download android studio kwa kutumia link chini kisha install kwenye computer yako
https://developer.android.com/studio/index.html

JavaSe (Java Development Kit)


programming language ambayo inatumika kutengeneza Android app ni Oracle’s Java SE. Java SE ilitengenezwa na Sun Microsystems na baadae ikanunuliwa na Oracle.
Zipo aina tatu za Java. Kuna Java EE (Java Enterprise Edition) ambayo hii hutumika kwenye network ya macomputer makubwa. Halafu kuna Java ME (Java Micro Edition) ambayo utumika kutengeneza mobile application. Java SE ina uwezo mkubwa kuliko Java ME na ndio inatumiwa na Google kutengeneza Android Os.
Ili kuweza kuweka JavaSe (Java Development Kit) kwenye computer yako unatakiwa kutembelea link chini kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa download. Hakikisha ume download na ku-install JavaSe (Java Development Kit) maana bila kufanya hivyo hutaweza kutengeneza android app.
http://www.oracle.com/technetwork/java/javase/downloads/index.html
Hivyo vitatu ndivyo vitu vya muhimu ambavyo una hitaji ili uweze kutengeza android applications.
As salaam aleykum wapendwa, Ukuwaji wa sayansi na teknolojia Umerahisisha mambo mengi katika jamii zetu na kuweza kutuletea ufanisi wa hali ya juu katika shughuli zetu za kila siku. Sasa unaweza kununua, kuuza bidhaa mbalimbali mtandaoni kulingana na mahali ulipo.
Unaweza kufanya manunuzi haya kupitia tovuti mbalimbali ambazo zinatoa huduma hii ya uuzaji na ununuaji wa bidhaa na huduma mbalimbali waweza sema ni soko huru la kimtandao. Inategemea wewe sasa unahitaji kutumia soko gani. Watu wengi  wanatamani kununua bidhaa kutoka kwenye maduka yaliyopo Marekani kama Amazon, Ebay, Best Buy, Walmart, Official stores za makampuni makubwa na mengine mengi ila hawajui wafanyeje.
Kuagiza bidhaa kwenye maduka ya mtandaoni yaliyopo marekani ni rahisi sana, kuna vitu vifuatwavyo vinahitajika.
  • Uelewa kuhusu usalama wa duka unalotaka kununua bidhaa.
  • Kuwa na Kadi ya benki iliyounganishwa na Visa au MasterCard.
  • Paypal account kwajili ya kufanya manunuzi mtandaoni
  • Kuwa na anuani ya marekani, kwa sababu sio maduka yote yanaweza kukutumia bidhaa au mzigo hadi Tanzania
  • Malipo ya Kodi Tanzania

Usalama wa duka unalotaka kununua

Hapa nadhani ndo watu wengi wanapoogopa. Ni kweli mtandaoni kuna utapeli, ila hili unaweza kulidhibiti kama ukipata bidhaa zako toka kwenye maduka makubwa na maarufu kama Amazonebaywalmart nk au kutoka kwenye maduka ya wazalishaji moja kwa moja kama Sony nk.
Ila kuna baadhi ya bidhaa hazipatikani katika maduka yenye umaarufu, hii haimaanishi kwamba hawaaminiki, sema hapa inabidi kujiridhisha binafsi kabla hujafanya manunuzi. Unaweza jiridhisha kwa kuwasiliana nao, kusoma reviews za watu wengine mtandaoni, nk.
Kuongezea usalama, nashauri malipo yapitie kwenye akaunti yako ya Paypal. Nitazungumzia jinsi ya kujiunga na huduma hii.

Jinsi ya kupata Visa/MasterCard Card

Ili uweze kufanya manunuzi online itabidi uwe na kadi ya benki iliyounganishwa na Visa au MasterCard systems. Visa na MasterCard ni mifumo ya malipo inayokuwezesha kutumia akaunti yako ya benki kufanya manunuzi katika nchi nyingi duniani.
Kadi ambazo zimeunganishwa na mifumo hii zinakuwa na nembo ya Visa au MasterCard kama zinavyoonyeshwa hapa chini.
Kadi hizi zinakuwa na card number yenye tarakimu 16 kwa mbele ya kadi, mwezi na mwaka wa kuexpire na CSC/CVV namba inakuwa na tarakimu 3 (hii ni kama password) hizo ndo utakazotumia kufanya malipo. Iweke kadi yako mahali salama na usimpe mtu hizi namba, maana zinatosha kufanya manunuzi.
Unapoomba kadi hii kutoka benki angalia inayokuwezesha kuweka U$D hii itakusaidia kutopata “exchange rates” mbaya wakati unanunua bidhaa mtandaoni, sababu bidhaa nyingi zinauzwa kwa dola. Kadi ambazo hazikuruhusu kuweka U$d  yaani za shilingi unaweza kuzitumia pia ila angalia ambayo haina makato makubwa sana wakati unanunua vitu.
Unaweza kutumia benki ya BancABCCRDB, EQUITY au benki nyingine zinazotoa kadi zinazoweza fanya manunuzi mtandaoni.

Paypal Account kwajili ya Kufanya Manunuzi Mtandaoni

PayPal ni biashara ya kimataifa ya kieletroniki (e-commerce) ya kuruhusu malipo na uhamisho wa fedha kufanywa kupitia mtandao. Uhamisho wa fedha mtandaoni hutumiwa kama njia mbadala ya kielektroniki ya kufanya malipo na mifumo ya kawaida, kama vile hundi na maagizo ya fedha (checks and money orders).
PayPal ni mfumo, unaofanya malipo kwa wauzaji wa mtandaoni, tovuti za mnada, na watumiaji wengine wa kibiashara, ambapo kufungua na kutumia akaunti hii kwa “malipo” ni bure , ila pale unapoanza “pokea” malipo kuna kuwa na gharama kidogo kuendana na kiasi kilichopokelewa.
Paypal akaunti itakusaidia kulinda taarifa za MasterCard au Visa zisiibiwe, kila mara unapofanya malipo, utakuwa unalipia kwa Paypal akaunti na si kadi yako. Na mfano ikatatokea umelipia kitu afu haujakipata unaweza ripoti tatizo na Paypal watakusaidia kutatua.
Ingawa kuna baadhi ya maduka hayasapoti malipo ya Paypal, ila asilimia kubwa ya maduka yanasapoti na nakushauri kufanya manunuzi kwenye maduka yanayosapoti Paypal, maana ni rahisi kurudishiwa Pesa yako pale utakapokuwa na tatizo na muuzaji, na pia ni njia salama ya kupambana na matapeli wa mtandaoni.
Ukishafungua akaunti na Paypal utahitajika kuunganisha kadi yako ya Visa/MasterCard na Paypal akaunti yako.
Paypal watahitaji kukuchaji nadhani $1 kwenye kadi yako ambayo watakurudishia ili kuweza kuunganisha kadi yako na account yako ya Paypal. Na utahitajika kuwapa nambari fulani ambayo inahusiana na hayo malipo ya $1 kwa ajili ya kuhakiki taarifa zako na kukuwezesha kuanza kutumia kadi yako.
Usijali Paypal watakupa maelekezo yote. Hii namba inayohusishwa na malipo ya $1 utaipata ukiwauliza benki waliyokupa kadi au kama una “online bank account” ya kadi yako utaweza kuiona hii namba.

Bidhaa Uliyonunua Inafikaje Tanzania

Hii ni mojawapo ya changamoto ya kuagiza bidhaa mtandaoni kutoka Marekani ni kuwa maduka mengi hayasapoti utumaji wa mizigo nje ya Marekani.
Kununua kutoka Ebay au Amazon unachotakiwa kujua ni makampuni yanayoaminika ya usambazaji wa vitu. Yanakusaidia kufanya ununuzi bila mipaka. Mengi hufanya kazi kwa kukupa anwani ya kipekee ya U.S kutumika kama anwani yako ya usafirishaji wakati unanunua bidhaa yoyote kutoka kwenye duka la U.S mtandaoni.
Duka hutuma bidhaa yako kwenye anwani yako ya U.S; kampuni inapokea bidhaa hiyo na kukuletea Tanzania kwa ada ndogo.

Kuna makampuni mbalimbali ya usambazaji lakini moja la kuaminika ni MyUS.com au Shipito kampuni hizi zinatumiwa na watu wengi wa Tanzania.
Ila hii huduma sio bure pia sio gharama kubwa ukizingatia kama kitu unachoagiza kina umuhimu kwako.

Malipo ya Kodi Tanzania

Mizigo ukipokea kuna kodi utachajiwa. Hii kodi itategemea na thamani ya mzigo iliyoandikwa kwenye risiti. Kodi unayotakiwa kulipa inafikaga hadi 50% ya thamani ya mzigo.
Kwenye akaunti yako ya Shipito au MyUs kabla hujatuma mzigo kuna fomu ya “customs clearance” unajaza, hii fomu ndo inabidi “uijaze vizuri tumia ujanja” kupunguza kiasi cha kodi utakacholipa. Pia unaweza wapa Shipito special request waondoe zile risiti za bei za mzigo na kuacha hii customs clearance fomu tu.
Swala la kodi ni gumu inabidi uwe umejipanga nalo. Ni vizuri kutumia USPS ili uweze “negotiate” kodi pale unapoenda pokea mizigo yako kwenye ofisi za Posta.

Hitimisho

Kuagiza bidhaa mtandaoni kutoka Marekani si ngumu kama watu wanavyodhani, ila changamoto kubwa ni gharama za utumaji mizigo kwenda Tanzania na gharama za kodi.
Kama una swali lolote tuandikie comment yako hapo chini au kama unataka wasiliana na sisi tuandikia kupitia fomu ya  “Wasiliana Nasi
As salaam aleikum warahmatullah wabarakatuh kipindi cha nyuma kidogo nilieza jinsi ya kupiga Ubuntu Fuatana nami ili uweze kupiga windows 7 katika mashine yako bila malipo yeyote

Ingiza CD yako katika DVD-ROOM ya mashine yako kisha subiri CD yako isome ikisha soma Restart mashine yako kisha bonyeza Boot Button, hapa kila mashine huwa zinatofautiana ila nyingi ni F8, F10 au F12, so angalia mashine yako boot button yake ni ipi.

Kama itagoma usichoke rudia tena ila ikikubali utaona kama pichani hapo juu
Fanya machaguo sahihi hapo katika Lugha, Time na type ya keyboard hiyo kwenye picha mimi ndo huwa naitumia wakati wote sijawahi kubadilisha, kisha bonyeza Next
Utaona muonekano kama huo juu pichani sasa bonyeza Install Now
Weka tiki katika kibox ili kukubaliana na sheria za microsoft kisha bonyeza next ili kuendelea
Bonyeza Upgrade kama ulikuwa na Windows 7 na unataka kuibadilisha...Au bonyeza Custom (advanced) huna Windows 7 na unaweka windows 7 upya

Chagua Drive kama ni (C:) AU (D:) ambayo unataka kuweka windows 7.Bonyeza  Drive options (advanced) kama unataka kutengeneza Partiton (Kuigawanya hard disk ) Kisha bonyeza Next, sasa windows yako itaanza mchakato wake wa kujiweka katika mashine yako tazama picha hapa chini.
Baada ya michakato hiyo mashine yako itajizima na kujiwasha usiogope bado ipo katika mchakato tazama picha hapa chiniIkishajiwasha itaendelea na mchakato wa setup iliyobakia itachukua muda kidogo wenda ikazidi ule muda wa mwanzo lakini usijali itamaliza kisha itajizima na kujiwasha kwa mara ya pili.


ikishawaka sasa itakupa chaguo la kuandika jina unaweza kuandika jina lolote ulipendalo pia ukipenda unaweza kuweka na Password lakini kama hautopenda andika jina tu kisha bonyeza next, wenda ikakuomba Keys chukua hapa kama hauna lakini pia unaweza kubonyeza next bila kuweka ila itakuja kukuomba baadae
Bonyeza next kisha set vitu hivi chini pichani kama utakavyopenda weweMpaka kufikia hapo tayari mashine yako kwa kutumika Imeandikwa na +Riyadi Bhai Picha zote kutoka Mtandaoni. kama hujaelewa au unaswali lolote kuhusu mada hii niachie maoni yako hapo chini. 


As salam aleikum ndugu zangu kutokana na huku mtaani kwetu kuwa na studio kibao zainazouza movie zilizotafsiriwa nimeonelea nikujuze wenda huwa unajiuliza hivi hawa jamaa wanatafsiri vipi fuatana nami mwanzo mwisho.

1. UJUZI WA LUGHA JAPO KIDOGO

Hili ni jambo bora zaidi maana hawa jamaa kina DJ wetu duh ni full shida unakuta mtu kasema Softdrink yeye anakutafsiria kuwa ni maji moto sasa hii inakuwa ni hatari  sana kabla hujafikiria kuwa mfasiri wa hizi movie hakikisha unafahamu unachotusimulia, pia kabla ya kuitafsiri movie  hakikisha umeitazama na kuielewa vema

2. hakikisha unakuwa na vifaa hivi

Tafuta GPU yenye CPU nzuri na RAM japo hata 4GB
Microphone japo ya Tsh 15000
pia Screen Recorder kama Ice Cream, Camtasia au yeyote utayoona ni nzuri zaidi kwa upande wako

3. jinsi ya kutafsiri sasa

Chomeka microphone yako katika mashine kisha install software yako ya screen recorder kisha fungua movie unayotaka kuitafsiri kupitia VLC au player yeyote kisha fungua software yako kisha mark au elekesha nafasi unayotaka kurecord kisha anza kurekodi wakati imeanza kurekodi basi anza kazi yako ya kutafsiri microphone kwa masaada mkubwa wa software yako sauti itabakia katika movie ukimaliza stopisha na utaisave kisha convert katika format unayoihitaji tayari kwa kuangalia movie yako katika lugha yako uliyoitumia.

sambaza makala hii kwa marafiki nao wafahamu ishu hii pia niachie maoni yako hapo chini, kama unahitaji kutumia makala hii katika mtandao wako soma hapa kabla ya kukopi https://riyadibhai.blogspot.com/p/about.html
As salaam aleikum kuna kipindi tuliongelea jinsi ya kutumia hotspot ya simu kwenda katika pc sasa leo tuangalie kutoka katika pc,laptop kwa wireless 

Kuna program fulani inaitwa Baidu Pc Faster (inahusika na optimization ya pc) download hapa


, then install kwenye pc yako..baada ya hapo ifungue, then uende kwenye Wi-Fi hotspot ambayo imechorwa ile alama ya Wi-Fi...fanya set up, yaani ipe jina na password..then save...


soma >>>jinsi ya kutumia modem kama hotspot

Baada ya hapo connect modem yako yenye line uliyojiunga kifurushi cha net, ikishasoma rudi kule kwenye hiyo program ya Baidu pc faster fanya kuenable/kuweka On hiyo wireless yako....Then serereka kwenye simu/tablet au pc yako...!
As salam aleikum ndugu yangu Kuna sababu nyingi sana zinazofanya WiFi unayorusha kutoka katika kifaa chako cha android kuwa slow sana. Moja ya sababu hizo ni uwezekano wa kifaa au mtu mmoja usiyemfahamu anatumia WiFi yako bila ya wewe kujua na akawa anakula data ya kutosha. Sasa leo tutaangalia jinsi ya kumkamata mwizi wa yako na kumfungia kabisa.

Nani anatumia WiFi yangu?

Kujua nani anatumia WiFi yako kitu cha kwanza ni kuhakikisha umejiunga katika WiFi husika. Kisha download app inayoitwa Fing kutoka katika Playstore au link hii hapa.
Baada ya kuipakua na kuifungua utaona jina la network yako pamoja na kitufe cha refresh, bonyeza kitufe cha refresh ili uweze kupata majina ya vifaa vilivyoungwa katika mtandao wako.
Baada ya muda, refresh itamaliza na hapo utaona orodha ya vifaa vyote vilivyoungwa katika mtandao huo pamoja na icon ya kuonyesha kama ni PC au ni Simu.
Bonyeza moja ya vifaa hivyo ili kupata menu ya jinsi ya kukimudu kifaa husika, kama PING au Wake On LAN signals na pia unaweza ukaset muda gani vifaa hivyo vijiunge katika WiFi yako na muda gani visijiunge.

Jinsi ya Kublock?

Kama utaona kifaa kigeni katik orodha yako unaweza ukakiblock moja kwa moja kutumia mtandao wako. Fing itakuonyesha MAC Address ya kila kifaa kilichoungwa katika mtandao wako.

Njia mbadala

Unaweza ukaend katika settings=>mobile networks=>tethering and portable hotspot na hapo utachagua WiFi Hotspot, orodha ya vifaa vilivyoungwa katika wifi yako vitaonekana hapo.
Kisha bonyeza kwenye kifaa husika kisha chagua Forget na hicho kifaa kitaondoka katika orodha yako.
Njia nyingine rahisi ni kuhakikisha unabadili passwords za WiFi yako mara kwa mara ili kupunguza uwezekano wa watu kutumia WiFi yako bila ya wewe kufahamu.

Usisahau Kulike Page yangu ya Facebook.


Pale unaponunua simu mpya, kinachofuata ni kuhamisha vitu vyako vyote kutoka katika simu ya zamani kama vile contacts, picha, video, baadhi ya apps na vitu vingine vingi. Lakini kuhamishi vitu vyote hivi huwa inachukua muda mwingi sana kama hutotumia njia sahihi za kufanya hivyo.

Hebu leo tuangalie baadhi ya njia sahihi na za haraka za kuhamisha vitu kutoka katika simu moja kwenda nyingine.

1. Kuhamisha Contacts

Contacts zako ni moja ya vitu muhimu zaidi katika simu yako. Zile enzi za kunakili contact zako zote pembeni na kuzisave upya katika simu zimepitwa na wakati.
A. Hamisha kwa kutumia SD Card
Funga sehemu ya Menu => Manage Contacts => import/export contacts. Hapa utaweza kuhamisha contacts kutoka katika simu yako ya zamani. Kuzisave katika simu yako mpya fuata step kama za hapo juu ila kwenye kuexport/import utachagua uzisave kwenye simu. Njia hii ni kwa wale wenye simu zenye sehemu ya kuweka slots za memory cards.
B. Hamisha kwa kutumia Account yako ya Google (Gmail)
Gmail wamerasisha zaidi zoezi la kuhamisha contacts kwa kuweka chaguo maalumu la contacts synchronization kwa vifaa vyote vinavyotumia account moja ya gmail.
Ili kuweza kutumia huduma hii inakupasa kutumia email account moja ya google katika vifaa vyako vyote. Kufanya hivyo nenda kwenye settings=>Accounts=>Google=>Add new Account kama haipo kisha katika sehemu ya synchronization weka on ili kuruhusu simu yako kushare contacts zake na simu nyingine zenye account kama hiyo.
C. Kuhamisha kwa kutumia laini ya SIM (SIM Card)
Hii ni njia ya kizamani japo inaendelea kusaidia watu. Faida kubwa ya njia hii ni uwezo wa kuchagua contacts zipi uhame nazo na zipi uziache. Unachotakiwa kufanya ni kuwa na SIM Card isiyokuwa na majina kabisa na kucopy majina yote kutoka katika simu yako ya zamani na kuyahamishia katika simu yako mpya.
Tatizo kubwa la njia hii ni uwezo wake mdogo wa kuhamisha contacts 200 tu kwa pamoja.

2. Jinsi ya kuhamisha SMS zako

Kama bado unazipenda baadhi ya sms zako kama za malipo ya bili mbalimbali, usitie shaka unaweza ukahama nazo pia kwa msaada wa app inayoitwa  SMS Backup and Restore ambayo inafanya kile ulichokitarajia. App hii ni ya bure kabisa na unaweza ukaipakua kutoka Playstore.

3. Jinsi ya kuhamisha picha, video na miziki

Hapa kuna njia nyingi kama vile kutumia SD Card yenye uwezo mkubwa kucopy na kuhamishia kwenye simu mpya au kutumia baadhi ya apps za cloud storage kama Google Drive, Google Photos au DropBox kuhamisha vitu vyako. Tatizo la njia hizo zinahitaji kiasi kikubwa cha data.
Hivyo kwa urahisi tumia kompyuta yako kuhamisha mafaili kwa kuyacopy kwenye kompyuta kwanza alafu kuyahamishia kwenye simu mpya.

4. Jinsi ya kuhamisha Applications na data zake

Hapa utahitajika uwe umeiroot simu yako. Sikushauri kufanya hivyo kwa simu yako mpya kwa sababu unaweza ukaharibu warranty ya simu yako. Baada ya kuiroot tumia application ya  Titanium Backup, app hii itakuwezesha kubackup kila kitu katika simu yako.

Chanzo : Swahilitech.com
As salaam aleikum ndugu zangu karibuni katika mtandao huu ili tuendelee kufahamishana mawili matatu kama ilivyoada, 

 ingia playstore download ppsspp app alafu, inakupasa kudownload winrar au easy unrar pia maana file za games zinabidi kubadilishwa kabla uja zifungua kwenye ppsspp 
 hizo app mbili ndizo zinazo kuwezesha kuplay ppsspp games kwenye simu yako ya android. 
 ukisha download app hizo mbili ambazo ni ppsspp na winrar
ingia google alafu tafuta games for ppsspp zitakuja website mbalimbali ingia moja ya hizo website ambazo zina games za ppsspp chagua game unayoipenda download file lake.
ukisha maliza ingia kwenye app ya winrar au easy unrar kisha tafuta file la game ulilo download ndani ya hiyo app ukishalipata limark "EXTRACT" hakikisha hadi lifinish and then click BACK.

Ukimaliza hatua hizo zote ingia katika app yako ya Ppsspp kisha tafuta file lako la game ulilo  EXTRACT NA WINRAR AU EASY UNRAR Utakuta picha ya game lako kama inavyoonekana pichani fungua na uplay
Back To Top