TRENDING NOW

Tangaza Nasi
As salaam aleikumndugu zangu kutokana na kila mmoja anakuwa na sheria zake kwaajili yake na watu wake binafsi nimeanzisha blog hii kwaajili ya kuwasaidia watu wa aina zote zaidi blogger's hasa wanaotumia lugha ya kiswahili lakini kwa masikitiko makubwa nimeona sheria zangu zikivunjwa wazi kabisa jambo ambalo likanatisha tamaa kuendelea kufanya mambo makubwa zaidi, nimeweka sheria kwa wale wanao kopi makala zangu hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/about.html nimeweka masharti rahisi sana katika sheria hiyo lakini watu wamekuwa wagumu kuelewa.

mpaka umeamua kukopi makala kutoka sehemu moja kupeleka kwako bila shaka umefahamu ni ugumu kiasi gani kuandaa makala mpaka ikiwa na msaada kwa watu wengine hivyo ili tusivunjane moyo katika kusaidiana naomba tujitahidi kufuata sheria za blog hii kwani sifanyi ili kupata pesa lakini nafanya hapa ili kuwasaidia watu wengine kama unahitaji kukopi makala kutoka katika blog hii soma hapa kabla ya kukopi https://riyadibhai.blogspot.com/p/about.html soma sheria za huduma zangu hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/terms-of-service.html soma sheria mama za mtandao huu hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/privacy-policy.html kama unamalalamiko soma hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/blog-page_29.html kama utakubaliana na sheria hizo basi wasiliana nami hapa https://riyadibhai.blogspot.com/p/contact.html
As salaam aleikum mpendwa msomaji wa swahilitech.net, GODMODE? wengi wanaweza wakakuona kama kichaa, hapana hii ni njia rahisi ya kupata mipangilio (settings) zote muhimu za Windows 10.
Kuna muda unatamani uwe na njia rahisi ya kupata mipangilio yote ya kompyuta yako bila kuhangaika sana. Usihofu, windows 10 ina njia moja rahisi sana ya kukusaidia  kupata shortcut za mipangilio yote ya muhimu maarufu kwa jina la GODMODE.

Fanya hivi, tengeneza folder mahali popote katika kompyuta yako isipokuwa katika desktop na lipe jina GodMode.{ED7BA470-8E54-465E-825C-99712043E01C} Basi hapo umemamliza, mara baada ya kusave folder hili utaona icon inabadilika, muda wowote unapofungua folder hili unapata mipangilio yote ya muhimu ya kompyuta yako.

Je, una swali lolote kuhusu mada hii? Uliza swali lako katika kisanduku cha maoni hapo chini.
As salaam aleikum mpendwa kama kawaida msomaji wangu kutokana na kutokuwa hewani kwa muda mrefu sasa ni muda wa kuweka makala za kutosha hadi tuombane po, wacha tuendelee Kulinda simu yako au tablet yako ya Android hakuishii kwenye kuweka screen lock tu, la hasha kuna njia nyingine nyingi za kuifanya simu na data zako kuwa salama muda wote.
Leo tujaribu kuangalia njia 10 zitakazokusaidia kuifanya simu yako iwe salama muda wote. Tumeamua kuanza na simu na tablet za android kwa sababu asilimia kubwa simu zinazotumika hapa Tanzania kwa sasa ni za Android.

1. Weka Screenlock
Kuweka lock kwenye screen yako ni njia moja ya muhimu ya kuilinda simu yako hasa pale unapoipoteza au unapoiacha kwenye mikono isiyo salama. Katika mfumo endeshi wa android unaweza ukaweka screen lock tofauti kama PIN lock, Pattern lock, Password lock au Fingerprint scanner kama simu yako inauwezo huo. Kuna baadhi ya matoleo unaweza ukaweka voice lock au eye scanner lock. Hii inamzuia mtu mwingine asiyehusika na simu yako kuweza kuifungua bila ridhaa yako. Kuset screen lock fungua Settings–> Security–> Screen lock na hapo utachagua inayokufaa.

2. Lock Application zako za msingi, picha pamoja na video
Unaweza ukaongeza ulinzi katika application zako ambazo hutaki mtu mwingine aweze kuzitumia au kuzifungua kwa kuzilock kwa kutumia baadhi ya application za kulock mafail na application kama App Lock inayopatikana googe play store. Hii itakusaidia sana kulinda taarifa zako za ndani hata kama mtu amefanikiwa kutoa screen lock yako.

3. Hakikisha Mfumo Endeshi wako (OS) pamoja na Application zote unazotumia zipo Updated
Hii ni ya msingi zaidi kwani wengi wetu tumekuwa tukipuuzia kupdate application zetu hata pale zinapotuomba kuziupdate. Makampuni yanayotengeneza application husika huwa wanaziupdate sio tu kuongeza vitu vipya au kuongeza ufanisi, hapana bali kuziba mianya yote ya kiusalama iliyoachwa wazi hapo kabla. Unatakiwa kuset simu yako iwe inaupdate application zake automatically pale tu zinapotoka kwa kufungua Settings–> General –>Auto update application ( Hapa inategemea na toleo la android unalotumia).

4. Usidownload Application nje ya Googleplay store
Kwa kawaida simu yako huwa haikuruhusu kudownload application nje ya play store, ila unaweza kubadilisha hili kwenye settings–> security–>Device Administration –> Unknown sources kiurahisi. Sasa sio vizuri kabisa kupakua application nje ya play store kwa usalama wa simu yako. Wadukuzi wengi wamekuwa wakitumia mwanya huu kuiba data za mwenye simu au hata kuiharibu simu yenyewe (Kwa wenye tecno Y6 na H6 watakuwa mashuhuda wa simu zao inafikia kipindi huwezi kuicontrol) . Kwa hiyo unatakiwa kuzima hiyo kama unajua unachokifanya na unauhakika na application unayotaka kuinstal.

5. Kuwa makini na Application Permissions wakati unapoziinstal
Hii ni ya muhimu na kuzingatia sana, mara nyingi huwa tunapoinstal application kutoka Google Play huwa zinaomba ruhusa ya kutumia baadhi ya vitu katika simu yako. Kwa mfano punde tu unapoanza kuinstall Whatsapp huwa inaomba ruhusa ya kusoma majina na namba za simu zako, kutumia kamera yako pamoja na kutumia kinasa sauti chako, mara nyingi huwa tunaziruhusu kwa kubonyeza allow. Sasa hapa ni kwa kuzingatia zaidi hasa unapojaribu kuinstal application ambazo zinaomba ruhusa ya kutumia namba zako za simu au picha zako, lazima uwe na uhakika na hiyo application kwanza.

Kwenye toleo jipya la Android Marshmallow unauwezo wa kuruhusu au kuzuia ruhusa kwa application hata kama tayari umeshainstall.

6. Kuwa makini na taarifa unazoshare
Simu nyingi za Android zinatumia kivinjari cha Chrome kama kivinjari cha kwanza, kivinjari hiki kina uwezo wa kutunza taarifa zako zote za kuperuzi na kuzituma katika vifaa vyako vyote unavyotumia kama vile Tablet, Laptop pamoja na desktop zenye kivinjari hichi. Passwords, bookmarks pamoja na vingine vya ziada kupitia Google account vinaweza kuwa shared kwa kukurahisishia kazi wewe mtumiaji. Ila jaribu kufikiri kama umepoteza simu na ina kivinjari cha Chrome chenye taarifa zako zote, inakuwa rahisi kwa mtu aliyeiokota au kuiiba kusoma au kunakili taarifa zako. Hivyo hakikisha unakuwa makini linapokuja suala la kuchagua ni aina gani ya taarifa unataka kushare na vifaa vyako vingine.

7. Kumbuka kuset Android Device Manager
Android Device Manager ni njia inayokusaidia kutafuta simu yako pale inapopotea au kuibiwa. Kwa kuwasha Android device Manager unakuwa na uwezo wa kufuta data zako zote pale simu yako inapokuwa imeibiwa au kupotea au kuipiga na kuilia kwa sauti. Jinsi ya kuwasha Android Device Manager, nenda kwenye settings–>Securty–>Device administration na hapo utaona kitufe cha kuwasha chaguo hilo.

8. Backup Data zako
Kubackup data zako ni jambo la muhimu la msingi sana hasa linapokuja swala la simu za mkononi au tablet. Kwa mfano kurusu Synchronization ya namba zako za simu kati ya kifaa chako na akaunti yako ya gmail ni jambo la msingi zaidi kwa sasa. hii itakusaidia hata pale unapoamua kubadilisha simu hautakuwa na haja ya kuandika upya contact zako, ni kitendo cha kuingiza email (barua pepe) yako na contact zako zote zitajisave. Pia ni muhimu kutunza data zilizomo kwenye simu yako katika kifaa kingine tofauti na simu yako. Kwenye matoleo ya Lollipop pamoja na Android Marshmallow mtumiaji anaweza akaset backup kwa kuingia tu kwenye settings za simu yake.

9. Jaribu kujikinga na Virusi vya Android pamoja na Malware
Siku hizi kuna mamilioni ya virusi vya kompyuta vimetapakaa mtandaoni, hii haishii kwenye kompyuta tu, hapana mpaka kwenye simu zetu kuna mamilioni ya virusi vinavyoweza kudhuru simu zetu huko mtandaoni na ni muhimu kujua njia fasaha za kujizuia na mashambulizi ya virusi hivi. Ndio wengi tunajitahidi kuinstall Antiviruses katika simu zetu kama vile Avast, Android au Kaspersky lakini hii si ya muhimu sana kwa sasa. Njia pekee na ya usalama ni kuepuka kuinstall applications nje ya Google Play store.

10. Set User Accounts
Kama imetokea simu yako huitumii peke yako, au kama wewe ni baba na simu yako huwa inatumika na watoto wako au mkeo kwenye kucheza magemu, ni vizuri kuset user accounts ili kuruhusu ni nani atakuwa na uwezo wa kufungua nini katika simu yako. Kuanzia toleo la Android Lollpop mtumiaji ana uwezo wa kuset user accounts bila wasiwasi wowote. Fungua Settings–>Users–>Add Users na hapo utaset kulingana na matakwa yako.


as salaam aleikum mpendwa, Zimebaki siku chache sana simu ya Samsung Galaxy S9 itoke na tayari kwenye mitandao mbalimbali kumefurika tetesi mbalimbali juu ya ujio wa simu hii, lakini je ni vitu gani vinategemewa kuja kwenye simu hii.?
Kupitia makala hii tutaenda kuangalia baadhi ya vitu ikiwa pamoja na sifa zinazo tegemewa kuja kwenye simu hii mpya ambayo imepanga kuzinduliwa rasmi siku ya jumapili ya tarehe 25 mwezi huu.


  • Kamera

Kwa kuanza tuanze na kamera ambayo ndio sehemu inayotegemewa kuangaliwa sana kwenye toleo hili jipya la Galaxy S9. Simu hii inatarajiwa kuja na kamera mbili za nyuma zikiwa na uwezo wa Megapixel 12 kwa Galaxy S9 Plus na kamera moja kwa Galaxy S9. Kamera hizi zimeboreshwa zaidi na kuongezewa uwezo wa kuchukua picha vizuri hasa wakati wa usiku au kwenye mwanga mdogo.
  • Ulinzi

Mbali na matoleo ya nyuma ya Simu za Galaxy, toleo hili jipya la Galaxy S9 linakuja na ulinzi wa aina mpya ambao unaitwa Intelligent Scan, ulinzi huu ni mchanganyiko wa sehemu muhimu za Facial Recognition pamoja na Iris Scanner zote zikifanya kazi kwa pamoja.
  • Ujio wa 3D emoji

Itakuwa kama ilivyo sehemu ya Animoj kwenye iPhone X na kutumia simu mpya ya Galaxy S9 utaweza kutengeneza Emoji zenye kutembea na kufanya kazi kama ilivyo kwenye simu ya iPhone X.  • Ujio wa Slow Motion
Hii ni sehemu ambayo itakuwa kwenye kamera na inategemewa kuongeza uwezo wa kamera ya Galaxy S9 kuchukua video za taratibu au Slom Motion.
Sifa Nyingine
Sifa zingine ambazo zinategemewa kuja kwenye simu hii mpya ya Samsung Galaxy S9 ni pamoja na kioo cha Inch 5.8 chenye teknolojia ya QHD na Super AMOLED curved display (570ppi / 529ppi), Processor ya Qualcomm Snapdragon 845 (kwa simu za  marekani) na Samsung Exynos 9810 (kwa simu za UK). Pia Samsung Galaxy S9 Plus inategemewa kuja na ukubwa wa ndani wa GB 128 na RAM ya GB 6  na Galaxy S9 itakuwa na ukubwa wa GB 64 na RAM ya GB 4.
Na hivyo ndivyo baadhi ya vitu vinavyo tegemewa kuja kwenye kwenye simu mpya ya Galaxy S9 pamoja na S9 Plus.
Je' unaionaje samsung s9 niachie maoni yako hapo chini
As salaam aleikum mpendwa msomaji wangu, Kuna siku nilikuwa naandika makala moja nzuri na ndefu kwa ajili ya kuipublish kwenye swahilitech, nikiwa kama page ya tano ghafla umeme ukakatika na nisijue nini cha kufanya sababu kazi yenyewe nilikuwa sijaisave (hifadhi) bado.
Nadhani hata wewe ulishawahi kukutwa na aina hii ya fedheha na ukashindwa kujua nini cha kufanya. Ondoa shaka leo nitakuelekeza jinsi ya kurudisha kazi yako uliyoifunga kwa bahati mbaya au kwa sababu ya kukatika kwa umeme katika Microsoft Word, Microsoft Publisher, Microsoft Excell pamoja na Microsoft Power Point. [soma : Activate microsoft office free download ]

Njia hii inafanya kazi vizuri zaidi kwa vifurushi (packages) za Microsoft Office 2010,2013  na 2016 kwa sababu kazi unayoichapa huwa inahifadhiwa kwenye draft bila ya wewe kujua. Unaweza ukaset muda wa kazi kuwa saved automatically katika Tab ya save, ila kwa kawaida huwa inakuwa ni dakika 10.
[soma : microsoft office professional plus 2016 product keys, serial keys 2017 ]
Njia za kufuata ili kurudisha kazi yako uliyoifunga kwa bahati mbaya katika moja ya bidhaa za Ms Office

  1. Fungua Microsoft Office uliyokuwa ukitumia kama ni Word, Excel, Publisher au Power point
  2. Bonyeza File Tab, upande wa kushoto juu kabisa, kisha bonyeza Recent
  3. Bonyeza Recover Unsaved Document kama upo kwenye Ms Word, na Recover Unsaved Workbook kama upo kwenye Excel na Recover Unsaved Presentation kama upo kwenye power point.
  4. Kazi yako iliyohifadhiwa kwenye draft itaonekana na utaifungua ili kuendelea kuiedit (kuifanyia kazi)
  5. Baada ya kuifungua sasa kumbuka kuisave ili kupunguza uwezekano wa kuipoteza tena pale umeme unapokatika.
Nadhani sasa utakuwa umefahamu jinsi ya kurudisha kazi yako iliyopotea kwa bahati mbaya, na kama ulikuwa unaandika makala au unachapa kazi ndefu nadhani una kila sababu yakufurahia.

sambaza upendo kwa kushare makala hii kwa washkaji ili nao wasihuzunike na hadha za kupoteza kazi zao
As salaam aleikum mpendwa leo tujifunze kuhusu whatsapp, Uharibifu ni moja ya sifa inayomfanya mwanadamu kukamilika, sio kila uharibifu unaofanya lazima uwe na madhara makubwa kwa jamii au mazingira. Leo nataka tujifunze jinsi ya kuharibu au kucrash WhatsApp ya rafiki yako.
Je, kuna mtu amekukera au anakukera katika whatsapp kwa kukutumia picha au jumbe usizozipenda na umejaribu kumuonya bila mafanikio? Fanya hivi, mtumia ujumbe mmoja wenye emoji 5,000 na herufi kadhaa hapo utakuwa umemaliza kila kitu.

Njia rahisi ya kufanya hivi ni kutumia whatsapp web ili uwe na uwezo wa kuandika emoji zote hizo kirahisi, baada tu ya kupokea ujumbe huo whatsapp yake itacrash na atashindwa kufanya lolote mpaka atoe hiyo whatsapp na kuweka upya kabisa (unistall).

Kwanini emoji 5,000 zinasababisha whatsapp kucrash? Ni hivi, whatsapp imetengenezwa kumudu jumbe zenye urefu wa herufi 6,000 tu hivyo kutuma emoji 5,000 kunaipa mzigo app hiyo na kuifanya icrash. Njia hii ni kwa whatsapp za katika simu za android tu na haifanyi kazi katika iphone.

Tumia mautundu haya kwa nia ya kujifunza tu. onyesha upendo kwa kushare makala hii kwa washkaji
As salaam aleikum mpendwa msomaji wa ukumbi huu, hakika kila mmoja wetu anapenda kumiliki simu kali tena simu janja ya kisasa, lakini wenda tunakosea wakati wa kufanya manunuzi, kwani sio kila simu inafaa kununua kuna nyingine ni matatizo hapa chini nimejaribu kukuelezea mambo ya kuzingatia wakati wa kununua simu


Epuka kuwa na haraka/pupa/ kukimbilia

Unapaswa kuepuka kuwa na haraka/pupa/kukimbilia kununua kitu ambacho utaweza kujuta baadae. Unahitaji kuchukua muda kufanya uchunguzi juu ya simu unayoitaka kabla ya kwenda kuinunua, sote tunajua haraka haraka haina baraka ukiwa na haraka itapelekea ukauziwa simu ya bei rahisi kwa pesa nyingi kutokana na kukosa umakini katika manunuzi yako.

Epuka ushindani

hasa kwa dada zangu, Hatupaswi kuwa na mashindano yoyote wakati wa kununua simu nzuri. Aina ya simu za mkononi ambazo wengine wanatumia hazipaswi kukuongoza kununua yako. Huna haja ya kushindana, sio lazima. Nunua kulingana na pesa zako zinazoweza kumudu, kwani unaweza kujikuta unashindwa kufanya mambo ya msingi kutokana na kufikiria kuwa na simu kama ya jirani yako wakati uwezo njaa zimekata break.

Epuka kununua smart phone iliyotumika

mwaka jana nikiwa kituo cha polisi rumande nilisikia mashtaka mengi kuhusu simu, kila aliyelalamika alijitetea kwa kusema kuwa alinunua kwa mtu yeye hausiki, Watu wengi hutumia au hununua simu ya mkononi iliyotumiwa na hatimaye kupata matatizo mengi baadaye. Ili kuepuka hili, unahitaji kununua simu (smart phone) ambayo ni mpya na inayoweza kudumu/kuishi kwa muda mrefu. Hasa kwenye uwezo wa betri.

Epuka kununua smart phone mitaani

Hili jambo siku hizi limezoeleka sana. Watu wengi wananunua smart phones mitaa kwa kigezo cha bei rahisi kisa simu anayoinunua imetumika kwa muda fulani. Wengi wa wanaouza smart phones mitaani ni walaghai na wanaweza kukupa simu mbovu na mbaya. Ni dhahiri kabisa wengi tushawahi kuuziwa simu mbovu mitaani. Ni vyema kujishauri na kufanya maamuzi sahihi kabla ya kununua simu huko mtaani ili kuepuka hayo matatizo hasa kutapeliwa.

Neno la Muandishi: sio simu zote zinazouzwa mitaani ni Fake au hazina Ubora ila ni vema ukanunua simu mpya.
As salaam aleikum ndugu yangu blogger mwenzangu au hata msomaji wangu natumaini wewe ni mzima mimi pia alhamdulillah, Katika zama hizi watu wengi sana wanamiliki blogs, za personal, entertainment au matangazo mbali, kila mtu akiwa na dhamira tofauti akilini mwake. Lakini sio Kila Blog inayoanzishwa inadumu, wengi hushindwa kufika mbali na hatimaye blogs zao hufa au kukosa wafuatiliaji.

Zifuatazo ni miongoni mwa sababu zinazosababisha Blog nyingi Kutofanikiwa:-


1.Kukosa Content zako Mwenyewe, hatimaye kuanza Ku Copy na Ku Paste.

Hili ni jambo ambalo Bloggers wengi wa Hapa kwetu Tanzania Wamelizoea, Ndio maana utakuta habari au makala ileile imeandikwa na Bloggers zaidi ya watano bila kubadilishwa kitu, hii hupunguza taswira ya umakini toka kwa wafuatiliaji wako.

2. Kukosa Ufuatiliaji katika Blogs/Sites zenye Muingiliano na Blog yako.

Kama umedhamiria blog yako iende mbele basi ni jambo la lazima kuwa unatembelea blogs zenye maudhui ya kufanana nawe ili upate changamoto kuhusu nini cha kufanya na kuandika.

3. Kujibu Maswali au Hoja zinazoulizwa sehemu nyingine ambazo hazijapatiwa Ufumbuzi.

Kama ni mtembeleaji wa blogs/sites nyingine unaweza ku observe ni kipi wafutiliaje wanakihoji na hakijapata majibu au maelezo ii wewe ndo iwe sehemu yako ya kujikusanyia wafuatiliaji kwa kuwapa wanachokihitaji.

4. Kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa.

Kama una nia ya dhati ya kufika mbali na Blog yako basi uwe mtu wa kujifunza mara kwa mara toka kwa waliofanikiwa ili nawe utembelea hatua zao katika kukwepa matatizo na kupata mafanikio.

5. Usijiache Peke yako tu, Jichanganye na Bloggers wenzio.

Hii pia ni tatizo kwetu, kwani kuna Bloggers ambao wao wanajiona ndio ma Top, basi hawana muda wa kuwasikiliza hawa wa chini wanaomba nini au ushauri gani wanataka, pia hata kuwawekea link za blogs zao ni shida, pia sisi tunaoanza ku blog tujishirikishe kwa wenzetu ili kukuza traffic na exposure.

Imeandikwa na KAJICHO KIVULI wa JF
As salaam aleikum, Zikiwa zimebaki siku chache kuzinduliwa kwa simu za Samsung Galaxy S9 na Samsung Galaxy S9 Plus inaelezwa huenda zikawa ndio toleo la mwisho la simu za familia ya S.

Kwa mujibu wa wachambuzi na watafiti wanaofatilia kwa karibu masuala ya simu janja wanasema hatua hiyo itakuja kwa ajili ya kupunguza urefu wa jina wa kuitwa S10 na badala yake toleo lijalo likaitwa “SX”. X itasimama kama namba 10 ni kama vile walivyofanya kampuni ya Apple kwa toleo lake la iPhone X.

Na kwamba inaelezwa matoleo yatakayofatia yatajulikana na kutofautishwa kwa mwaka wa simu ilivyotolewa. Yaani itakuwa Galaxy X (2020), Galaxy XI (2021) na kuendelea lakini hili wachambuzi wa masuala ya simu janja wameliona kutowezekana kwa Samsung kufanya hivyo kwani itakuwa ngumu kutofautisha baina ya toleo moja kwa jingine.
Hata hivyo, vyanzo vinasema Galaxy X itakuwa ni mwisho wa familia ya S na hilo pia litajiri kwa familia ya matoleo ya Note ambayo pia inakaribia toleo Note 9 kutoka mwaka huu. Simu mpya ya Samsung inayotarajiwa kutoka kati ya mwaka 2019 yenye uwezo wa kukunjwa na kujikunjua pamoja na kuwa na vioo viwili inaelezwa itakuwa na jina la Samsung Galaxy X.  Kujua undani wa simu ya Samsung itakayokuwa na vioo viwili BOFYA HAPA.


Hakuna uhakika kama simu hiyo ndio itahitimisha matoleo ya S au la!. Mvuto wa jina na urahisi wake pia huchangia kwa bidhaa kufahamika kirahisi kwa wateja na kununulika kwa wingi. Endelea kutembelea SwahiliTech.net, tutakujulisha mara moja kama kutakuwa na mabadiliko…

As salaam aleikum. Je, unakumbuka simu za mkunjo za kipindi cha miaka ya 90 na 2000? Kama ndio basi zimerudi tena lakini katika kiwango cha ubora wa juu, muonekano wa kuvutia zaidi pamoja na teknolojia ya kisasa.

Kampuni ya Samsung ikishirikiana na China Telecom imetangaza uzinduzi wa simu ya bei ghali ya mkunjo yenye vioo viwili inayofahamika kama Samsung W2018.

Uzinduzi wa simu janja hiyo umefanyika Desemba mosi mwaka jana huko Xiamen, nchini China ukiambatana na sherehe za kutimia miaka 15 ya toleo la familia ya W kwa simu za Samsung Galaxy na miaka 25 ya soko la Samsung nchini China.

Samsung W2018 ambayo sifa zake za ndani inafanana sana na Sansung Galaxy S8, inakuja na kioo cha ukubwa wa nchi 4.2 chenye teknolojia ya AMOLED pamoja na RAM yenye ukubwa 6GB na ukubwa wa uhifadhi wa ndani wenye ukubwa wa 64GB na 256GB.
Uzuri wa simu hii utaweza kutumia aidha kioo cha nje au ndani baada ya kuikunjua simu yako. Mfano unaweza kutumia kioo cha ndani na ukabadili kwa kutumia kioo cha nje kwa kazi ileile iliyokuwa kwenye kioo cha ndani na ukaendelea nayo ama ukaendelea na kitu kingine kipya.

Pia itakupa na uwanja mpana wa kutumia baobonye/kicharazio (keyboard) halisi au ya kugusa (Touch).

Ukubwa wa Betri katika Samsung W2018 ni 2,300mAh na itakuwa na mfumo endeshi wa Android Nougat. Simu hiyo itakuwa katika rangi nyeusi, Fedha na Dhahabu.

Kwa upande wa kamera kutakuwa na kamera ya nyuma yenye 12MP na kamera ya mbele yenye 5MP na kuweza kurekodi video kwa teknolojia ya 4K. Simu hiyo itaendeshwa na  prosesa ya Snapdragon 835.

Hata hivyo kikwazo kikubwa cha simu hiyo ni bei yake. Kama ulidhani iPhone X ni ghali zaidi, basi kwa Samsung W2018 ni ghali zaidi.

Ingawa bei haijawekwa rasmi lakini inaelezwa bei ya Samsung W2018 itauzwa kwa Dola za kimarekani 2,400 ambazo ni takribani Tsh 5,399,040 ambazo pesa hizo zinamuwezesha Mtanzania wa kawaida kumudu kununua kiwanja cha ukubwa mzuri kilichopimwa na serikali.

Hii sio simu janja ya kwanza ya Samsung Galaxy kuwa ya mkunjo. Simu janja ya mkunjo nyingine ilizinduliwa mapema mwaka huu inayofahamika kwa jina la Samsung leadership 8 ambayo nayo inapatikana kwa soko la China pekee.

Simu ya Samsung W2018 kwa sasa itapatikana katika soko la China pekee na hakuna taarifa rasmi kama itapatikana katika masoko mbalimbali katika nchi zingine.

Nini maoni yako kuhusiana na makala haya. Je una swali lolote. kwa maoni au maswali kuhusu makala haya usisite kutuandikia hapo chini nasi tutakujibu haraka iwezekanavyo.